Baadhi ya maafisa wa jeshi la utawala wa Kizayuni
wa Israel wameishauri Marekani kuwa haipasi kundi la kigaidi la Daesh
(ISIS) litokomezwe kwa sababu kundi hilo halijawahi kuwa tishio na
hatari kwa Israel.
Katika makala iliyoandikwa na Zuhair Andraos kwenye gazeti la Al Ra'ayul-Yaum
linalochapishwa London, Uingereza mwandishi huyo ameeleza kuwa kundi la
kigaidi na ukufurishaji la Daesh halijafanya shambulio lolote la
kijeshi dhidi ya Israel au kulenga maslahi ya Israel na wazayuni ndani
na nje ya mipaka ya utawala huo haramu.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, hivi karibuni aliyekuwa Waziri wa Vita wa
utawala wa Kizayuni wa Israel Moshe Ya'alon alifichua kuwa magaidi wa
kundi la ukufurishaji la Daesh waliwahi mara moja kuwashambulia kimakosa
askari wa utawala huo katika eneo la miinuko ya Golan kusini mwa Syria
lakini waliomba radhi haraka.
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
0 Maoni:
Post a Comment