Jeshi la Yemen na vikosi vya wananchi wa nchi hiyo
vimejibu uchokozi na jinai za Saudi Arabia na washirika wake kwa
kuwaangamiza wanajeshi saba wa Saudia.
Kanali ya Televisheni ya
al-Masirah imeripoti kwamba, jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya
wananchi wa nchi hiyo vimefanya mashambulio dhidi ya kituo kimoja cha
kijeshi cha Saudia kilichoanzishwa hivi karibuni huko Najran kusini mwa
nchi hiyo ambapo mbali na kufanya uharibifu mkubwa vimewaangamiza
wanajeshi saba wa nchi hiyo.
Aidha makumi ya wanajeshi wa Saudia wanaripotiwa kujeruhiwa katika mashambulio hayo huku hali ya baadhi yao ikiwa mbaya.
Saudia kwa kushirikiana na Marekani,
Israel, Uingereza na baadhi ya nchi za Kiarabu, ilianzisha mashambulizi
ya kichokozi nchini Yemen mwezi Machi mwaka 2015 ambapo katika hujuma
hizo zaidi ya watu elfu 12 wamepoteza maisha. Hii ni katika hali ambayo
Saudia na washirika wake hao wameshindwa kufikia malengo yao ya
kumrejesha madarakani kwa nguvu kibaraka wao, Abdrabbuh Mansur Hadi rais
wa zamani wa Yemen aliyejiuzulu na kutoroka nchi.
0 Maoni:
Post a Comment