Serikali
imetangaza kuanzia June 2 hadi 4, 2017 Watanzania wataingia bure katika
Mbuga na Hifadhi za Wanyama nchini kote ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya Siku ya Mazingira Tanzania ambayo yatafanyika kitaifa Butiama mkoani
Mara.
Waziri
wa Mazingira na Muungano January Makamba amesema tayari utaratibu
umeshafuatwa ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Wizara ya Maliasili na
Utalii pamoja na TANAPA kuwa katika siku hizo tatu Watanzania wataingia
bure katika Mbuga na Hifadhi za Wanyama.
Maadhimisho
ya siku ya mazingira duniani kitaifa yanatarajiwa kufanyika June 5
mwaka huu Butiama Mkoani Mara huku kukitarajiwa kuwa na mijadala
mbalimbali itakayojadiliwa kuhusu utunzaji wa mazingira.
Akizungumza
na wanahabari jana, waziri wa wizara hiyo, January Makamba alisema
lengo la kupeleka maadhimisho hayo Butiama ni kumuenzi Nyerere ambaye
alikuwa mwanamazingira namba moja nchini sanjari na kukumbuka mchango
wake katika masuala ya uhifadhi wa mazingira nchini.
Kwa
mujibu wa Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli Mkoani Tanga, kauli mbiu
ya maadhimisho ya mwaka huu nchini ni utunzaji wa mazingira na maendeleo
ya viwanda.
0 Maoni:
Post a Comment