Polisi Uingereza walalamikia picha za Manchester

Picha za shambulio zilizochapishwa na gazeti hilo Picha za shambulio zilizochapishwa na gazeti hilo

Polisi nchini Uingereza wameyalaumu machapisho yaliyotolewa katika gazeti la New York Times juu ya picha na taarifa kutoka katika eneo ambalo shambulio la bomu lilitokea mjini Manchester.

Maafisa nchini humo wanasema kuvuja kwa picha hizo kuna haribu uchunguzi wa polisi na kuondoa imani na washirika wao katika masuala ya kiintelejinsia.

Picha hizo zinaonesha vitu mbalimbali ambavyo vingetumika kama ushahidi kama vile betri na vitu vingine vyenye muonekano wa vilipuzi.

Hata hivyo gazeti hilo la Marekani limejitetea juu ya picha hizo ambazo imesema zinaashiria kuwa bomu lililotumika katika shambulio hilo kwa kiasi kikubwa linaonekana kuwa ni la kisasa.

Waziri mkuu wa Uingereza anatarajiwa kulipeleka suala hilo kwa Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa Jumuia ya NATO, ambao unafanyika leo.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment