Wachezaji wa Ghana wakishangilia baada ya mchezo kumalizika
Timu za vijana za Ghana na Mali
zimefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika
chini ya umri wa miaka 17.
Ghana wametinga fainali baada ya kupata
ushindi wa penati 6-5 dhidi ya Niger baada ya kwenda sare katika
dakika tisini za mchezo.
Mabingwa watetezi Mali wao
wamefanikiwa kutinga fainali yao ya pili mfululizo baada ya
kuwaondosha Guinea kwa penati 2-0 huku kipa wa Mali Youssouf Koita,
akiwa shujaa wa timu hiyo kwa kuokoa michomo mingi na penati
Wachezaji wa timu ya Mali
Mchezo wa fainali ya michuano hiyo ya vijana utapigwa jumapili ya
tarehe 28 mchezo ukichezwa katika dimba la AmitiƩ Sino-Gabonaise, mjini
Libreville,
Mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Niger na
Guinea nao utafanyika siku hiyo hiyo ya jumapili katika uwanja wa
katika uwanja AmitiƩ Sino-Gabonaise.
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
0 Maoni:
Post a Comment