Siku moja baada ya mchezaji nyota wa
gofu Tiger Woods kukausha kuwa hakuwa amelewa wakati polisi
walipomkamata siku ya jumatatu, taarifa za polisi zinasema kuwa mchezaji
huyo alikutwa amelala ama (amezima) wakati injini ya gari ikiwa
inafanya kazi.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Woods mchezaji wa zamani namba moja kwa ubora duniani, alikutwa katika usukano wa gari yake aina ya Mercedes na aliamshwa kwa dakika kadhaa na afisa wa polisi aliyemuona
Alikamatwa kwa kosa la kuendesha chombo cha moto akiwa amelala lakini alikanusha hilo na kusema kuwa ni matokeo ya dawa kali anazozitumia baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo.
0 Maoni:
Post a Comment