Mahrez aomba kuondoka Leicester City

Mahrez amekuwa na mchango mkubwa ndani ya klabu ya Leicester City 
Kiungo wa Leicester City Riyad Mahrez amesema kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo.

Mchezaji huyo mwenye miaka 26 aliyejiunga na klabu hiyo akitokea Le Havre ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho wa paundi 400,000 mwaka 2014, amesema alikubali kubaki klabuni hapo kwa msimu mwingine baada ya majadiliano mazuri na mwenyekiti walipoishangaza dunia kwa kuwa mabingwa wa EPL msimu uliopita.

Lakini kwa sasa amesema kuwa tiyari amekwisha iambia klabu juu ya kuondoka kwake na anaomba wamruhusu kufanya hivyo.

Mahrez mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa England mwaka 2016, amecheza mara 48 msimu huu akifunga magoli 10 na kutoa pasi saba za magoli.

Leicester ilianza msimu wa ligi ya England vibaya na hatimaye kumaliza katika nafasi ya 12, lakini ikafika hatua ya robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment