Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, askari watatu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa waliuawa na wanane kujeruhiwa katika shambulizi la Jumatatu 9 Mei kusini mwa nchi hiyo. Askari mmoja hajulikani alipo.
Msafara wa magari ya Kambodia yakilindwa na askari wa Umoja wa mataifa kutoka Morocco ulikua ukitokea Rafai ukielekea Bangassou, miji miwili ilio kwenye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Msafara huyo ulishambuliwa usiku wa Jumatatu katika eneo la Yogofongo, kilomita ishirini kutoka Bangassou. Katika urushianaji risasi kati ya watu wenye silaha na askari wa UN, askari mmoja wa Kambodia aliuawa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya Umoja wa Mataifa, shambulizi hilo liliendeshwa na wanamgambo wa Kikristo wa kundi la Anti-Balaka, ambao walikimbilia msituni baada ya shambulio. Baada ya shambulio hilo askari watatu wa Kambodia na mmoja kutoka Morocco walikosekana na kisha miili mitatu ya askari hao kupatikana.Askari wanne bado hajapatikana.
Askari wa UN walengwa na mashambulizi
Katika miezi ya hivi karibuni, eneo la kusini mwa jamhuri ya Afrika ya Kati limeendelea kukabiliwa mapigano kati ya makabila.
Katika mapigano hayo ya kikabila ambayo yanalikumba eneo lote la kusini mashariki mwa nchi, kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Minusca kimekua kikilengwa.
0 Maoni:
Post a Comment