Mkufunzi wa klabu ya Manchester
United Jose Mourinho anasema kuwa atawapumzisha wachezaji wake katika
mechi ya siku ya Jumapili dhidi ya Arsenal.
Huku kikosi hicho cha Mourinho kikiwa katika nafasi ya tano katika jedwali la ligi ya Uingereza, ligi ya kombe la Europa inaweza kuwapatia fursa ya kushiriki katika kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao.
''Wachezaji ambao wameshiriki katika mechi nyingi hatawachezeshwa wikendi'', alisema Mourinho.
Mpira wa dhabu wa Marcus Rashford uliipatia United ushindi katika awamu ya kwanza ya mechi ya marudio nchini Uhispania huku awamu ya pili ikitarajiwa Alhamisi ijayo katika uwanja wa Old Trafford.
0 Maoni:
Post a Comment