Dawa za Wanajihad zanaswa Uholanzi

Dawa za Wanajihad zanaswa Uholanzi
Maafisa wa polisi wa Uholanzi wanawatafuta washukiwa wawili baada ya maabara ya dawa kupatikana na furushi moja la dawa zinazopendwa sana na wanajihadi.
Maafisa hao walikuwa wamebaini walikuwa wamegundua dawa bandia za Capton na kusema hawajui iwapo zilikuwa zikipelekwa mashariki ya kati.
Wakati huohuo maafisa wa maswala ya fedha walifichua wiki hii wamefanikiwa kunasa dawa milioni 37.5 aina ya Tramadol ambazo hutumiwa na wapiganaji wa IS.
Mzigo huo ulikuwa unaelekea Libya.
Dawa aina ya Tramadol hutumiwa sawa na wapiganaji wa Boko haram nchini NigeriaMaafisa wa polisi wa Itali wanasema kuwa mzigo huo ulikuwa umetoka India na ungetumika kwa sababu mbili: Kusaidia kufadhili ugaidi na matumizi kwa wanajihad ili kujisisimua na kukabiliana na shinikizo la kiakili.
Utumizi wa Tramadol ulielezewa na ripoti kuwa wa kiwango cha juu miongoni mwa wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria na huenda ilitumika katika kusababisha mauaji katika pande zote mbili za mzozo.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment