Barcelona: Ernesto Valverde ateuliwa kuwa meneja

Ernesto Valverde 
Barcelona wamemteua Ernesto Valverde kuwa mkufunzi wao mkuu kwa mkataba wa miaka miwili, ambapo anaweza akaongezewa mwaka mwingine wa tatu.

Valverde ni mshambuliaji wa zamani wa Barca na alitangaza wiki iliyopita kwamba angeacha kazi Athletic Bilbao baada ya kuwaongoza kwa miaka minne.

Anachukua nafasi ya Luis Enrique aliyetangaza Machi kwamba angeihama klabu hiyo iliyomaliza nafasi ya pili La Liga msimu huu.

Anaondoka baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka mitatu.

Enrique aliongoza Barcelona kushinda mataji matatu makuu msimu wake wa kwanza, mataji mawili makuu ya nyumbani mwaka 2016 na Kombe la Mfalme au Copa del Rey mwaka huu.

Walilaza Alaves 3-1 mechi yake ya mwisho kuwa kwenye usukani katika fainali ya Kombe la Mfalme Jumapili.

Rais wa Barca Josep Maria Bartomeu alimsifu Valverde, 53, kwa uwezo wake, ufahamu, ujuzi na busara na kusema: "Huwa anaendeleza wachezaji chipukizi na hucheza mtindo wa Barca."
Valverde atazinduliwa rasmi kama meneja wa Barca Alhamisi.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment