Klabu ya Huddersfield Town
imepandishwa daraja kucheza Ligi ya Premia kwa mara ya kwanza baada ya
kulaza Reading 4-3 kupitia mikwaju ya penalti uwanjani Wembley Jumatatu.
Baada
ya kutoka sare 0-0 dakika 120, Town walitakiwa kupiga mikwaju kwa mara
ya pili na walikuwa na bahati tena baada ya kulaza pia Sheffield
Wednesday kwa mikwaju ya penalti hatua ya nusufainali.
Christopher
Schindler aliwashindia Town baada ya mkwaju wa Liam Moore kupaa angani
nao mpira wa Jordan Obita ukaokolewa na kipa Danny Ward.
Klabu hiyo ya Yorkshire Magharibi haijacheza soka ya ligi kuu tangu 1972.
Reading,
waliomaliza alama nne na nafasi mbili juu ya Town waliokuwa nafasi ya
tano katika ligi ya Championship sasa wameshindwa katika fainali ya
muondoano ya kufuzu kwa EPL baada ya ligi kwa mara ya nne.
Reading walimaliza nafasi ya tatu kwenye jedwali ligi ya Championship, alama nne juu ya Huddersfield
Aaron Mooy alikuwa mchezaji bora wa mechi na mmoja wa wachezaji wa Huddersfield waliofunga mikwaju yao Wembley
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
0 Maoni:
Post a Comment