Kocha wa Arsenal Arsene Wenger
amefanya mkutano muhimu na mmliki wa klabu hiyo Stan Kroenke Jumatatu
ambapo mustakabali wa mfaransa huyo ulitarajiwa kujadiliwa.
Bado haijajulikana kama Wenger ataongeza mkataba baada ya kudumu katika klabu hiyo kwa miaka 21.
Masharti ya mkataba mpya yalikubaliwa miezi kadhaa iliyopita, lakini hakuna kilichofanyiwa kazi mpaka hivi sasa.
Mipango ya Wenger ilikuwa kuendelea kubaki katika klabu hiyo lakini hali ilibadilika hivi karibuni baada ya kupingwa na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo.
Kumaliza pia nje ya timu nne bora na kukosa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao imekua changamoto kwake.
Lakini hali kidogo imekua shwari baada ya kuifunga Chelsea 2-1 katika fainali za kombe la FA siku ya Jumamosi na kumfanya Wenger kuwa kocha mwenye mafanikio zaidi kwenye kombe hilo huku Arsenal nayo ikiwa na mafanikio zaidi kuchukua kombe hilo.
0 Maoni:
Post a Comment