
Tezi dume ni ugonjwa unaopatikana katika njia ya mkojo ndani
ya mwili wa binadamu na mara nyingi huwapata wanaume wa miaka kuanzia 40 na
kuendelea.
Ugonjwa huu umekua ukishika kasi kwa hivi karibuni kutokana
na wanaume wengi kupatikana wakiwa na huu ugonjwa ambao umekua gumzo kwa miaka
ya hivi karibuni ambapo wanaume wengi wenye umri wa mtu mzima kuanzia miaka 40
na kundelea wameripotiwa kuwa na tatizo hili.
Watu wengi hawana uelewa wa ugonjwa huu na huku wengine
wamekua wakisema tezi dume ni sawa ugonjwa aina ya Busha huku wengine pia
wakiwa na imani potofu kua ugonjwa huu hupatikana kwa kurogwa.
Daktari Mseleto Nyakiroto ni Daktari bingwa wa magonjwa ya
upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoani Iringa ambaye MATUKIO DAIMA
ilifika ofisini kwake kuweza kufahamu juu ya ugonjwa huu wa tezi dume ambao
umekua gumzo miaka ya karibuni na ulianza kufahamika zaidi baada ya Mh Rais
Mstaafu DR Jakaya Mrisho Kikwete mwaka
2014 kuupata ugtonjwa huo na kwenda kutibiwa huko nje ya nchi nchini Marekani.
“Tezi dume si ugonjwa ila Tezi dume linapopata tatizo ndio
hutokea huo ugonjwa na huwapata zaidi wanaume ambao hupatikana katikati ya
kibofu na njia ya mkojo ndani ya mwili wa mwanume na linapovimba mgonjwa hupata
shida ya kuweza kukojoa na wakati mwingine huziba kabisa na mkojo kushindwa kupita”.
Alisema Dr Nyakiroto.

Daktari amebainisha sababu mbalimbali ambazo zinasababisha
kuupata ugonjwa huu ambayo ni homoni za mwanaume zikiwa kwa wingi sana husababisha
ugonjwa wa Tezi Dume huku pia kurithi kutoka baba mzazi huweza kusababisha mtu
kuweza kupata ugonjwa huu na dalili zake Nyakiroto anaeleza ni kua na matatizo
yakushindwa kukojoa vizuri na usiku mgonjwa anakua anakojoa mara kwa mara na
hasa kwa watu wazima wakuanzia miaka ya 40 huku wengine wakichelewa kwenda
hospitali njia za mkojo huziba kabisa na kushindwa kukojoa .
“Matibabu ya ugonjwa wa tezi dume hutegemea kulingana na
hali mhusika na kua kama atakua na uvimbe atafanyiwa upasuaji yaani Operation
na kwa wale ambao hawana uvimbe hua tunawapa dawa tu na kuwarusu kwenda
majumbani kwao kuendelea kutumia dawa”. Alisema Dr Nyakiroto
Nyakiroto anaeleza njia ya kubaini tatizo baada ya mgonjwa
kuwafikia ambayo mara nyingi watu wengi wanashtuka
na wengine kugoma kabisa kupimwa kutokana na aina yenyewe ya upimaji wa gonjwa
huu wa Tezi dume kuwa hutumia njia ya haja kubwa kubaini tatizo kwa kuingiza
baadhi ya vifaa eneo hilo na kubaini tatizo lakini pia njia nyingine ya kubaini
tatizo hilo ni kutumia mashine ya Ultrasound ambayo hupiga picha sehemu yenye
tatizo.
Aidha Nyakiroto anaeleza tofauti kati ya ugonjwa wa Tezi
dume na Busha na kua tezi dume hutokea ndani ya mwili wa mwanaume katikati ya
njia ya mkojo na kibofu na huwapata watu wa umri zaidi ya miaka 40 huku Busha
ni ugonjwa unaopatikana maeneo mengi ya Pwani na husababishwa kwa kungw’atwa na
mbu ambao hupatikana maeneo hayo ya pwani na ugonjwa huu huonekana kwa macho
kwani upo katika korodani za mwanaume punde mwanaume anapopata ugonjwa huu
korodani zake huvimba kutokana na kujaa maji.
Idadi ya wagonjwa waliopatikana Mkoani Iringa wenye ugonjwa
wa tezi dume tangu mwaka 2016 hadi sasa wamefikia wagonjwa 33 na wote waliweza
kutibiwa na wakaweza kupona tatizo hilo.
Sawa na hilo Myakiroto amewaomba wanaume wenye umri zaidi ya
miaka 40 ambao wanazo dalili ambazo ameeleza waweze kufika hospiatalini ili kuweza kuwapata matibabu kwani ugonjwa
huo unatibika kabla hawajapata madhara makubwa zaidi.
0 Maoni:
Post a Comment