Shauri La Kagera Sugar Halilali

Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji ya TFF inataraji kutoa maamuzi ya shauri la klabu ya Kagera Sugar inayopinga kupokwa pointi tatu na kamati ya saa 72 ifikapo mishale ya saa 11 jioni kwa saa za hapa nyumbani Tanzania.
Mkurugenzi wa vyama na uwanachama wa mikoa wa TFF, Eliud Mvela muda huu amezungumza na waandishi wa Habari ambao wamejitokeza kwenye kikao hicho akiwataka kuwa na subra au kwenda kuendelea na majukumu yao kisha kurejea muda huo wa saa 11 kwa ajili ya kufahamu kilichojiri ndani ya kamati hiyo.

Mvela alisema kamati imeamua kutoa maamuzi kwa muda huo baada ya kuona kuwa kuna mlolongo mrefu ambao utachukua muda zaidi.

Kikao hicho cha kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji kilianza kulijadili swala hilo kuanzia mishale ya saa nne asubuhi.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment