TAIFA la Marekani limesema sasa uvumilivu dhidi ya Korea Kaskazini umefika kikomo. Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence aliyasema hayo alipotembelea eneo ambalo haliruhusiwi kuwa na wanajeshi katika mpaka wa Korea Kaskazini na Korea Kusini. Ziara yake imetokea kipindi ambacho hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katika eneo la Korea, huku Marekani na Korea Kaskazini zikijibizana vikali.
Makamu huyo wa Rais, aliwasili mjini Seoul juzi saa chache baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la kurusha kombora, ambalo hata hivyo halikufanikiwa. Jana nchi za Marekani na Korea Kusini zilifanya mazoezi ya pamoja ya majeshi yake ya wanahewa, ikiwa ni jitihada za kuhakikisha wanajeshi hao wanakuwa tayari kwa tishio lolote litakalotokea Korea Kaskazini.
Pence ambaye baba yake alipigana katika Vita vya Korea, alihutubia wananchi katika Kijiji cha Panmunjom jana. Katika kijiji hicho ndipo mkataba wa kumaliza vita vya Korea ulitiwa saini. “Kumekuwepo na kipindi cha subira, lakini kipindi hicho cha subira sasa kimemalizika. Marekani inataka kuhakikisha kuna usalama Korea na inataka hilo lifanyike kwa njia za amani na majadiliano,” alisema. Walinzi wa Korea Kaskazini walifuatilia ziara ya Pence katika kijiji hicho kutoka mpakani na mmoja alionekana akipiga picha. Katika ziara hiyo, Pence pia alizuru eneo la Camp Bonifas, ambalo ni kambi ya kijeshi ya Umoja wa Mataifa karibu na eneo lisiloruhusiwa
0 Maoni:
Post a Comment