Askofu
Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dr. Josephat Gwajima jana
alijitokeza hadharani mbele ya waumini wa kanisa lake na kumtaka Halima
Mdee Mbunge wa CHADEMA kumuomba radhi Spika wa Bunge Job Ndugai kwa
maelezo kuwa alimtukana. Gwajima alisema, kama hatafanya hivyo, basi
ataitumia Jumapili Ijayo 'kumchapa' Hadharani
Kutokana na madai hayo, Halima Mdee amejitokeza hadharani na kumjibu Gwajima kupitia ukurasa wake wa Twitter nakusema kuwa,,
"Namuheshimu
sana Mch. Gwajima,sitajibizana nae kwenye mitandao. Niweke rekodi sawa
sijamtukana na wala sitarajii kumkosea heshima Spika.
"Hayo
ya J2 namwachia yeye! Yangu na yaliyojiri Bungeni.. Najua jinsi ya
kuyahandle. Yawezekana yalishamalizwa kabla ya Ibada yake LEO."
0 Maoni:
Post a Comment