
Msafara wa
wakala wa misitu
Tanzania TFS umevamiwa
katikati ya msitu na
wananchi wa kijiji
cha Mau kata ya
Mbuluma wilaya ya kalambo mkoani Rukwa kisha
gari la msafara
huo yenye namba
za usajili T. 8212 STK kupigwa mawe na
huku mafisa wa misitu
wakipotenea chuchupu kuambulia
kipigo.
Tukio hilo
la kushangaza limetokea
katika kijiji cha
Mau na kuvamiwa
na wananchi wa
kijjiji hicho kwa mawe na marungu na kuharibu
gari la msafara huo .
Akiongea na Mtandao huu ofisini
kwake mara baada
ya tukio kutokea meneja
wa misitu TFS wilayani
humo, Samweli Matula
amesema tukio hilo
limetokea wakati maafisa
misitu wakiwa wanaelekea doria , ambapo wakiwa
kijijini hapo walivamiwa
na kundi la
wananchi ambao walikuwa
wamebeba mkaa na kuvamia gari
lao kwa mawe
na kupelekea maafisa
wake kukimbia kwa
kuhofia usalama wa
maisha yao.
Amesema baada
ya tukio kutokea
walitoa taarifa polisi ambao
walifika mapema eneo
la tukio na
kukuta gari likiwa
limevunjwa vioo kwa mawe .
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
0 Maoni:
Post a Comment