Samwel Kambole (64) amenusurika kifo baada ya kujika kata uume wake
baada ya kupatwa na hasira nyingi zilizo tokana na misingo ya
mawazo inayo mkabili.
Akisimulia kutokea kwa mkasa huo kwa mashariti ya kuto
chukuliwa sauti yake mwenyekiti wa kitongoji cha Kotazi kijiji cha Kate
Richard Mselema amesema kuwa mtu huyo aliamua kujikata katika sehemu zake
za siri akidai kuwa usiku wakati amelala alimuota usingizini mke wake
ambaye ni marehemu kwa sasa akifanya naye tendo la ndoa.
Amesema baada ya kuamka asubuhi hakumuona tena mkewe aliyemuota usiku na
akichanganganya na matatizo mengine yanayomkabili aliamua kuuchukua uamuzi
wa kuanza kuukata uume wake kwa kutumia wembe na baada ya kupata
maumivu makali aliamua kupiga kelele za kuomba msaada.
Amedai kuwa kele hizo ziliwashitua wakazi wa kitongoji hicho na kwenda
eneo la tukio na kukuta mtu huyo akiwa amejichinja katoka sehemu zake za
siri ambapo walitoa taarifa katika kituo kidogo cha Polisi cha Kate na
kupewa PF3 na kukimbizwa katika zahanati ya Mission ya Kate kwa matibabu.
Mganga wa zamu katika zahanati hiyo Paul Katindi amekiri kumpokea mgonjwa
huyo na kuwa wao kama wauguzi walichukua hatua za haraka kumpatia matibabu
mgonjwa huyo ambapo jitihada zao ni kama ziliweza kuzaa matunda kwa kuweza
kuyaokoa maisha ya mtu huyo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Nkasi Zeno Mwanakulya ambae pia ni
kaka mtu na kijana huyo, amethibitisha kutokea kwa tukio na kusema
chanzo ni misongo ya mawazo kutokana na siku za hivi karibuni
kufiwa na mkewe pamoja na kupokonywa mashamaba yake yote na
ndugu zake kisha kuayauza bila ushirikishwaji na kusema kijana
huyo alitumia kifaa aina ya wembe kutoa uume wake.
0 Maoni:
Post a Comment