MKAZI
mmoja wa kijiji cha loesha kata ya Mbuluma wilaya ya
Kalambo mkoani Rukwa Regani Kakusa miaka 32 ameuwawa na watu
wasio fahamika kwa kukatwa na shoka sehemu za kichwani kisha
kufariki dunia hapo papo kutokana na wivu wa kimapenzi.
Diwani
wa kata hiyo saidi manoti magesa ,amesema mtu au watu wasio
fahamika walimvamia kijana huyo kisha kumkata na shoka
sehemu za kichwani na kupelekea umauti wake kumfika.
Kamanda
wa pilisi mkoani Rukwa Geoge Simba Kyando , amesema Chanzo cha
kufanya mauaji hayo ni wivu wa mapenzi ambapo inasadikiwa kuwa marehemu
alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa mtuhumiwa na kusema Mbinu
ilotumika kufanya mauaji hayo ni kwamba mtuhumiwa alimvizia kwa nyuma
marehemu wakiwa wameongozana kuelekea mnadani.
Aidha
kamnada kyando amesema Kamand ametoa ushauri kwa wananchi hususani
wanandoa kuwa waaminifu katika ndoa zao hata pale panapotokea
kutokuelewana waende katika taasisi za serikali zinazohusika na masuala
ya ndoa ili waweze kutatuliwa matatizo yao kisheria zaidi na sio
kuchukua maamuzi magumu ya kuua ambapo ni kosa la jinai kujichukulia
sheria mkononi.Aidha ameahidi kumsaka mtuhumiwa popote alipo ili aweze
kushukuliwa hatua stahiki za kisheria.
0 Maoni:
Post a Comment