Kocha maarufu Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ amesema, watani zao Yanga hawana tofauti na gari la maiti, la kwanza kuondoka la mwisho kurudi akimaanisha kwamba, wakati wa kwenda kwenye mazishi gari linalobeba maiti hutangulia kwenda makaburini halafu waombolezaji wanafata. Wakati wa kurudi wambolezaji wanatangulia kurudi halafu gari litafata nyuma.
Julio ambaye kwa sasa ni mshauri wa Simba Yanga lazima wafungwe kwenye mchezo wa Jumamosi kwa sababu Simba wanamuendelezo mzuri wa matokeo katika mechi kadhaa za hivi karibuni huku akijitapa kwamba, yeye (Julio) hajawahi kufungwa na Yanga tangu akiwa mchezaji na kocha wa Simba.
“Yanga kwetu kama gari ya maiti, ya kwanza kuondoka yamwisho kurudi. Lazima wafungwe, hakuna mjadala,” – Julio.
“Tulianza mechi na Majimaji tukafanikiwa, tukaja mechi na Prisons tukafanikiwa, tumefanikiwa dhidi ya African Lyon kwenye FA Cup na sasa tunakuja kwenye mechi ngumu dhidi ya Yanga.”
“Mimi kama Julio, nikiwa Simba kama kocha sijawahi kufungwa na Yanga na wala nikiwa mchezaji sijawahi kufungwa na Yanga.”
“Kwa hiyo niwatoe wasiwasi wanasimba kwamba sasa tunakwenda kwenye hotuba ya Nyerere ‘kuungana kwa wazungu’, Nyerere alisema wazungu wanaungana sasa Simba tumeungana ili tuhakikishe tunapata ushindi kwenye mchezo wetuwa Jumamosi tukiamini safari tukiwafunga Yanga shuhuri ya ubingwa tumemaliza.”
Julio pia alikuwa Zanzibar ambako Simba waliweka kambi kujiandaa na mchezo wa Simba vs Yanga Jumamosi hii.
0 Maoni:
Post a Comment