‘Hatujawahi kufungwa na Yanga mechi ikichezeshwa kwa haki’ – Manara



Afisa habari wa Simba amesema waamuzi waliopangwa kuchezesha mechi ya Simba na Yanga wachezeshe mechi hiyo kwa haki, huku akisema Simba haijawahi kufungwa na Yanga kama mechi ikichezeshwa kwa haki.

“Haijawahi kutokea hata siku moja Yanga wakatufunga mechi ikichezeshwa kwa haki, tukifungwa kihalali wote tutaridhika na nitakuwa mtu wa kwanza kuwapongeza, lakini figisu za namna yoyote safari hii hazita vumilika” – Haji Manara.

“Hii ni big match, ni mechi ya nchi, mechi inayochukua hisia za watu. Matarajio yetu ni kuona fair game kutoka kwa marefa, likipatikana hilo Yanga tunawafunga tu, hakuna mashaka yoyote tutawafunga tu ilimradi marefa waje kuchezesha mpira kwa haki.”

“Lakini marefa wakija na maamuzi yao, tunaomba serikali chini ya Rais Magufuli serikali iseme kitu mechi ya Simba na Yanga inabeba hisia za watu, sisi tunataka fair tu. Hatutaki kubebwa wala kupendelewa kwa namna yoyote tunachotaka mchezo uchezeshwe kwa haki.”

Kuhusu TFF kuchelewa kutaja waamuzi wa mechi hiyo, Manara alisema: “Mpaka sasa bado kuna figisu za kutaja waamuzi, nini kinaogopewa? Wapi umeshawahi kuona hadi yamebaki masaa 48 marefa bado hawajatajwa? Kwa nini nisiweke alama ya kuuliza? Kwa nini nisijiulize maswali milioni moja kichwani kuna nini kinaendelea? Tunataka wamuzi waje wachezeshe mpira kwa haki.”

“Viti vikivunjwa au watu wakiumia watalaumiwa viongozi wa Simba? Wakati hadi leo bado wa amuzi hawajatajwa, kuna tatizo gani, waamuzi watajwe nchi ijue kila mtu ajue.  Yanga inatayarishiwa nini hapa?  Hatukubali na haitotokea safari hii”.

“Simba ina ukubwa kuliko Yanga na mmeona, Simba ndio super brand ya nchi kwa hiyo lazima iheshimiwe kwa ukubwa wake.”
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment