Siku za Wayne Rooney kuwa United inaonekana zinahesabika.Ujio wa Mhiktaryan,Zlatan Ibdahimovich na Athony Martial unaiweka nafasi ya Rooney katika timu hiyo kuwa mashakani.Umri wa Rooney umeenda na kiwango kimeshuka na hii inamfanya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Man United.
Rooney ameshawahi sana kuhusishwa kuondoka Man
United,haijaanza leo kwa Rooney kuhusishwa na uhamisho wa kuondoka
United,kama umfuatiliaji mzuri wa masuala haya utakumbuka msimu wa
mwisho wa Alex Ferguson Wayne Rooney alihusishwa na uhamisho wa kwenda
Chelsea japo jambo hilo halikutokea.
Lakini sasa tetesi za Rooney kuondoka Man United
zimepamba moto sana.Wakati wa dirisha dogo la usajili la January
kuliibuka tetesi za Wayne kuhamia ligi ya China.Japokuwa klabu ambayo
ilikuwa ikihitaji huduma ya Wayne Rooney haikutajwa kwa kipindi hicho
ila ilikuwa ni wazi kwamba Wayne angevutwa China kutokana na nguvh kubwa
ya kifedha ya timu za nchi hiyo.
Tianjin Quanjian timu inayonolewa na nahodha wa zamani
wa Italia Fabio Cannavaro imekiri kuwahi kufanya na Rooney
mazungumzo.Cannavaro amekiri walimuhitaji Rooney japokuwa hafiti katika
staili yake ya uchezaji ila walijaribu kutaka kumsajili Wayne Rooney.
Tianjin Quanjian bado wanapewa nafasi kubwa kumnunua
Rooney,japokuwa wanasema katika mipango yao ya usajili jina la
mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Aubemayang ndio liko
juu.Tianjin pia wako na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina
Nikola Kalinic ili kuweza kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.
Kocha wa Man United Jose Mourinho amezidi kukuza tetesi
za Rooney kuondoka baada ya kukataa kueleza kuhusu usajili wa
Rooney.Mourinho aliwaambia waandishi wa habari kama wanataka kujua
kuhusu masuala ya Rooney kuondoka United baasi wakamuulize Rooney
mwenyewe.Kauli hiyo ya Mourinho imetafsiriwa kama kukosa uhakika kubaki
na Rooney msimu ujao.
Dirisha la usajili nchini China linaisha siku ya Jumanne
ijayo.Wakala wa Wayne Rooney aitwaje Paul Steford amesafiri hadi China
kujaribu kufanya mazungumzo na baadhi ya timu ikiwemo Tianjin.Tayari
Wachina wapo tayari kumlipa Rooney £600,000 kwa wiki kiasi ambacho ni
mara mbili ya mshahara wa sasa anaopokea.
0 Maoni:
Post a Comment