Na BARAKA
LUSAJO
MAMLAKA ya
usimamizi wa usafiri wa
majini na nchi
kavu {SUMATRA} katika wilaya
ya kalambo mkoani
Rukwa imesema imejipanga
kuendesha msako mkali
wa kuwasaka madereva wa usafiri wa pikipiki malfu kama bodaboda
ambao wamegoma kulipia
ada ya vyombo
vyao vya usafiri
sambamba na kupiga
malfuku watoto chini ya
umri wa miaka
{9} hadi sufuri {0} kubebwa kwenye
pikipiki.
Tamko hilo
linakuja kufutia siku
za hivi karibuni madereva
wa usafiri wa pikipiki malfu kama
bodaboda wilaya ya kalambo mkoani Rukwa
kugoma kulipia tozo
ya shilingi ishirini
na mbili elfu {22000/= ambayo
ilikuwa imetolewa na
mamlaka ya usafiri
wa majini na
nchi kavu {SAMATRA} kama ada ya
mwaka .
Hali hiyo
imefanya mamlaka ya usimamizi
wa usafiri wa
majini na nchi
kavu {SUMATRA} wilayani
humo kukaa kikao katika
ofisi za wilaya
hiyo na kutoa
tamko la kuendesha
msako mkali dhidi
ya madereva wote ambao wamegoma
kulipia tozo ya
fedha hizo na
huku ikidai kuwa mgomo wao ni
batili kutokana na madai
yao kuto kuwa
na mashiko kama anavyo
bainisha afisa biashara
wa wilaya hiyo Imani
Anangisye Mwasambyela.
0 Maoni:
Post a Comment