NA BARAKA LUSAJO
WALIMU
na wanafunzi katika shule ya msingi kipanga kata ya Samazi
wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wameingia kwenye hali ya
sintofahamu baada wananchi kugeuza eneo la vyunga vya shule
kuwa eneo la mazishi na kupelekea makaburi kuenea kuzunga
majengo ya shule hiyo na huku walimu wakilazimika kusitisha
masomo wakati wa mazishi.
Kutokana
na kujitokeza kwa malalamiko ya muda mlefu kutoka kwa walimu
na wanafunzi dhidi ya wananchi kugeuza eneo la vyunga vya
shule ya msingi kipanga kuwa la kufanyia mazishi ya watu
ambao wamekuwa wakifariki kwenye kijiji cha kipanga na katili
na kupelekea wanafunzi kuathiriwa na kelele aambazo huambatana
na vilio wakati wa mazishi ambayo yamekuwa yakifanyika
kuzunguka majengo ya shule hiyo kwa madai ya kijiji hicho
kuwa na ufinyu wa maeneo.
Hali
hiyo imefanya uongozi wa kata hiyo kuitisha kikao cha
wazazi na walezi na kufanyika shuleni hapo baada ya
kujitokeza kwa malalamiko na sintofahamu kutoka kwa walimu na
wanafunzi juu ya makaburi kujazana na huku kelele za mazishi
zikiwathiri wanafunzi wakati wa masomo na kupelekea uongozi wa
kata hiyo kupiga malfuku kufanya mazishi shuleni hapo.
Wazazi
na walezi kwa upande wao wamesema chanzo cha kufanya
mazishi shuleni hapo ni kutokana na ufinyu wa maeneo .
Mratibu
elimu kata Daudi sengo ambae akiongea kwa njia ya smu
amesema antegemea kukaa na wazazi ili kutafuta eneo mbadara
la kufanyia mazishi ili kuwafanya wanafunzi kusoma bila bugudha.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho Pus Mbauta amekili kuwepo adha hiyo na
kusema serikali ya kijiji imeanza kufanya utaratibu wa
kununua maeneo mengine kwa ajiri ya mazishi.
0 Maoni:
Post a Comment