Watu watatu
wa familia moja katika
kijiji na kata
ya mfinga Tarafa
ya mto wisa wilaya
ya Sumbawanga mkoani
Rukwa wamefariki dunia baada
kukatwa katwa na mapanga
katika sehemu mbalimbali
za mili yao kutokana na
imani za kishirikina.
Tukio hilo
la kushangaza limetokea
baada ya watu wasio
julikana kuwavamia watu hao nyumbani
kwao na kisha kuvunja mlango wa
nyumba yao na
kuwakatakata na mapanga na
kutokomea kusiko fahamika
kutokana na imani za
kishirikina.
Kamanda wa
polis mkoani Rukwa geoge
samba kyando amesema chanzo
cha tukio ni
imani za kishirikina ambapo
watu hao walivunja
mlango kisha kufanya
unyama huo na
kuwataja marehemu kuwa
ni JOACHIM KAYANDA ,umri miaka 60,EVERINA
MWANAKATWE ,umri miaka 47 na EMMANUEL KAYANDA, umri miaka 27 wote wakiwa ni
wakazi wa kijiji cha Kipa na kusema Watuhumiwa watano wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi na watafikshwa mahakamani pale
uchunguzi utakapokamilika.
0 Maoni:
Post a Comment