Kati ya watu wazima wanne na watoto watano mmojawapo ana dalili za ugonjwa wa akili kwa mujibu wa takwimu zilizofanywa na wataamu wa afya ya akili katika kipindi cha mwaka jana.
Akizungumzia mtaalamu wa afya ya akili katika Wilaya
ya Iringa vijijini Dkt Bruno O. Ndunguru
Alisema kuwa wagonjwa wa akili wamekuwa wakibaguliwa na kunyanyaswa na jamii
kutokana na imani potofu hususani kutokana na
sababu zinazosababisha magonjwa ya akili pamoja na kutofahamu kuhusu
matibabu ya magonjwa ya akili.
Alisema kuwa magonjwa ya akili yanasababishwa na
vyanzo vya afya mbaya ya akili ikiwemo kijamii ambapo inaambatana na matukio
katika maisha mfano kufiwa, kupoteza ajira na kisaikolojia mtu anashindwa
kupambana na misongo pamoja na uwezo mdogo wakujiamini wakati huohuo kimaumbile/kimwili hii ni
kutokana na sababu za
kurithi,lishe duni,magonjwa ya
kuambukiza na madhara yatokanayo na
kupata ajali.
“tunaamini kuwa kila binadamu ana kumbana na vitu vingi sana sasa unaposhindwa kuhimili vile vishindo katika
maisha yako baadae unaweza ukaishia kuchanganyikiwa na pia homoni zinapopungua
au kuongezeka zinaweza kusababisha
magonjwa ya akili kwahiyo ziwe za
wastani”alisema
Pia Dkt alifafanua kuwa magonjwa ya akili ni magonjwa yanayoathiri akili na kusababisha
usumbufu mdogo au mkubwa katika mawazo na mwenendo au tabia na matokeo yake
hupelekea kushindwa kukabiliana na mahitaji/shughuli za kawaida za maisha.
Aidha alisema kuwa magonjwa ya akili yapo ya aina
nyingi na mengi huwa hayatambuliki kwa urahisi kwa jamii na hata kwa watoa
huduma wa afya na hivyo wagonjwa wengi huchelewa kupata matibabu stahiki.
Alisema zipo dalili zinazoashiria magonjwa hayo ya
akili ikiwa ni pamoja na kihisia,
kimwili, na kiakili ambapo binadamu ana
kosa furaha na kuhuzunika sana,kuwa na furaha kupita kiasi,wasiwasi ,hasira za
haraka hadi kufikia kupiga wengine
kusahau kwa haraka kukosa
usingizi na msongo wa mawazo.
“kunywa pombe kupita kiasi mtu anaweza kunywa pombe
na kulala bar pamoja na kujitenga
ukiziona
dalili hizo jua una ugua magonjwa ya akili “alisema Dkt.
Sambamba na hayo alisema kuwa magonjwa ya akili
yanatibika ikiwa ni pamoja na tiba za kisaikolojia,dawa mbalimbali za
kutibu magonjwa ya akili, shughuli za kazi ambazo zinamsaidia mgonjwa
kutengemaa ufanisi wake.
Hata hivyo Dkt Ndunguru alisema kuwa kwa upande wa wilaya ya iringa
vijijini wameanzisha clinic ambayo ipo katika hospitali ya Ipamba kata ya
Kalenga na inasaidia kuwahudumia
wagonjwa wa akili pamoja nakuendelea kutoa elimu katika jamii jambo litalosaidia
kupunguza dhana potofu juu ya magonjwa hayo.
Alisema kuwa endapo mtu anaumwa na akapima hana
ugonjwa wowote jua kuwa ana matatizo katika ubongo wake na hivyo anashauriwa
kumuona daktari wa magonjwa hayo ili apate tiba haraka iwezekanavyo.
Ameiomba serikali pamoja na wadau wa mbalimbali kuwekeza kwa wingi katika kitengo cha magonjwa ya akili kwani kimesahaulika hali inayopelekea kukwamisha kitengo hicho kutopiga hatua.
0 Maoni:
Post a Comment