MADEREVA
wa usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda katika wilaya ya
Kalambo mkoani Rukwa wamegoma kulipia tozo ya shilingi elfu
ishilini na mbili {22000/=} iliyotangazwa na mamlaka ya
usimazi wa usafiri wa majini na nchi kavu {SUMATRA} kama ada
ya vyombo hivyo kwa mwaka kwa madai ya tozo hiyo kuwa kubwa
ukilinganisha na kipato chao.
Hatua
hiyo inakuja baada ya mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa
majini na nchi kavu {SUMATRA} siku za hivi karibuni kuwataka
madereva wa usafiri wa pikipiki malfu kama bodaboda kulipia
tozo ya shilingi elfu ishirini na mbili {22000} kwa mwaka
kama ada na huku ikiwataka kufikia February 28 ,2017 wawe
wamelipia , hali ambayo imepingwa vikari na madereva hao .
Hali
hiyo imefanya madereva hao kuitisha kikao cha pamoja ili
kujadiri swala hilo , ambapo wamegoma kulipia tozo hiyo
kwa madai ya mamlaka hiyo kuto washikirisha ikiwemo kutoa
elimu sambamba na tozo hiyo kuwa kubwa ukilinganisha na kipato
chao.
Mwenyekiti
wa madereva wa bodaboda wilayani humo Mwendo mwaluswaswa ,
amesema chanzo cha mgomo ni kutokana na malaka hiyo kuto
washirikisha wakati wa maamuzi .
Hali
imefanya kituo hiki kukutana na afisa biashara wa wilaya
hiyo Bakari Abdara , ambae licha ya kukili kuwepo adha hiyo
amesema wanategemea kua na madereva hao tarehe February 17
mwaka huu ili kumaliza mgogoro huo.
0 Maoni:
Post a Comment