Real Madrid yaweka rekodi ya mechi 40 bila kushindwa

Wachezaji wa Real Madrid wakumbatiana na kocha wao Zinedine Zidane baada ya sare ya 3-3 dhidi ya Sevilla 
Wachezaji wa Real Madrid wakumbatiana na kocha wao Zinedine Zidane baada ya sare ya 3-3 dhidi ya Sevilla  
 
Real Madrid imeweka rekodi mpya ya kushiriki mechi 40 bila kushindwa baada ya bao la dakika 93 la Karem Benzema kusawazisha na kusababisha sare ya 3-3 dhidi ya Sevilla katika kombe la Copa del Ray. 

Mara ya mwisho kwa kikosi cha Zinedine Zidane kushindwa ilikuwa dhidi ya Wolfsburg katika kombe la vilabu bingwa Ulaya katika awamu ya kwanza mnamo mwezi Aprili mwaka uliopita.
Barcelona ilikuwa inashikilia rekodi ya awali ya mechi 39, iliowekwa chini ya uongozi wa kocha Luis Enrique kati ya mwaka 2015 na 2016.

Sare hiyo ya siku ya Alhamisi inamaanisha kwamba Real imefuzu katika robo fainali ya kombe la Copa del Rey kwa ushindi wa 6-3 kwa jumla.

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Juventus, Real na Ufaransa Zidane mwenye umri wa miaka 44 aliteuliwa mnamo mwezi Januari 2016 baada ya kusimamia wachezaji wa ziada katika timu hiyo.

Kufikia sasa ameshinda mataji mengi ikilinganishwa na mechi aizopoteza -akiwa mshindi wa kombe la vilabu bingwa Ulaya, kombe la klabu bingwa duniani, kombe la Uefa Super Cup na kushindwa mara mbili pekee.

Real imeshinda mara 31 na kupata sare katika mechi tisa tangu ishindwe , na kufunga mabao 115 huku ikifungwa mabao 39.

Barcelona ilishinda mechi 32 na kupata sare 7 katika mechi zote kati ya mwezi Oktoba mwaka 2015 na Machi 2016.

Walishinda kombe la ligi mara mbili msimu huo.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment