Kama unatumia smartphone ya kizamani kutuma ujumbe wa WhatsApp, jipange kununua ya kisasa sababu unaweza usiweze tena kufurahia huduma hiyo.
WhatsApp imetangaza kuwa haitofanya kazi tena kwenye baadhi ya simu za kizamani hadi mwishoni mwa mwaka huu. App hiyo imetangaza kutozisupport tena simu zinazotumia mifumo ya zamani ya Windows, Android na Apple hadi January, na Blackberry na Nokia hadi kufikia katikati mwa 2017.
Ni kwasababu simu za kizamani, hazitoweza kukubali mabadiliko yatakayoongezeka kwenye app hiyo. WhatsApp imetoa tangazo hilo wakati ikisherehekea kutimiza miaka 7 tangu ianze kufanya kazi mwaka 2009.
App hiyo kwa sasa inatumiwa na watu zaidi ya bilioni 1 duniani.
Kupitia Website yake, WhatsApp imetaja simu itakazoziacha kuwa ni pamoja na zinazotumia mfumo wa Android 2.1 na Android 2.2; Windows Phone 7 na iPhone 3GS/iOS 6. Na hadi June 2017, WhatApp haitopatikana kwenye BlackBerry 10; Nokia S40; na Nokia Symbian S60.
0 Maoni:
Post a Comment