Bao pekee la kiungo Ibrahim Mohamed ‘MO’ limeendelea kuifanya Simba ibakile kileleni kwa tofauti ya pointi nne (4) mbele ya wapinzani wao Yanga SC walioshinda jana December 28 kwa bao 4-0 dhidi ya Ndanda FC.
Ushindi wa Yanga dhidi ya Ndanda, ulifanya mabingwa hao watetezi kuisogelea Simba kwa tofauti ya pointi moja wakati huo Simba ilikuwa haijacheza mchezo wake wa 18.
Kwahiyo ushindi wa Simba unafanya tofauti ya Simba na Yanga kuwa ni ileile ya pointi nne baada ya timu zote kucheza idadi sawa ya mechi.
Katika michezo nane iliyopita, Ruvu Shooting imeambulia sare moja huku ikiwa imepoteza mechi saba mbele ya ‘mnyama.’
Matokeo ya leo yanaifanya Simba ifikishe jumla ya pointi 44 kileleni mwa VPL huku Yanga ikifata nafasi ya pili kwa pointi zake 40 ikiwa timu zote zimeshacheza mechi 18.
0 Maoni:
Post a Comment