Vyombo zaidi ya 5,000 vimerushwa kwenye mzingo wa dunia na kuacha taka nyingi
Japan imezindua chombo cha anga za juu ambacho kitabeba mtambo maalum wa kukusanya taka kutoka anga za juu.
Chombo hicho kitakuwa na nyaya ndefu za urefu wa mita 700 (nusu maili) ambazo zitatumiwa kuokota taka hizo. Nyaya hizo zitaundwa kwa madini ya aluminiamu na chuma cha pua.
Mtambo huo umeundwa kwa usaidizi kutoka kwa kampuni ya uvuvi.
Inakadiriwa kwamba kuna zaidi ya vipande 100 milioni vya taka kwenye mzingo wa dunia.
Vipande hivi ni pamoja na vipande vya setilaini zilizoacha kutumika, vifaa na vipande vya roketi.
Vipand vingi kati ya hivi vinasonga kwa kasi sana kuizunguka dunia kwenye mzingo wake, baadhi vikifikia kasi ya kilomita 28,000 kwa saa (maili 17,500 kwa saa) na kuna wasiwasi kwamba vinaweza kusababisha ajali mbaya au kuharibu mitambo inayosaidia mawasiliano duniani.
Taka hizo zimerundikana katika kipindi cha miaka 50 tangu binadamu aweze kuruka kwenya anga za juu, setilaiti ya Sputnik iliporushwa anga za juu na Muungano wa Usovieti mwaka 1957.
Mgongano kati ya setilaiti na kufanyiwa majaribio kwa mitambo ya kujikinga dhidi ya mshambulio ya setilaiti vimezidisha tatizo la taka anga za juu.
Chombo hicho cha Japan kimepewa jina Kounotori na kinaundiwa katika kituo cha anga za juu cha Tanegashima
Roketi ya H-IIB iliyobeba chombo cha Kounotori ikipaa angani baada ya kurushwa kutoka kituo cha anga za juu cha Tanegashima tarehe 9 Desemba
Chombo hicho kilichopewa jina Kounotori (Korongo kwa Kijapani) na ambacho kimebebea mtambo huo, kilipaa kutoka kituo cha safari za anga za juu cha Tanegashima, kaskazini mwa bahari ya Pasifiki Ijumaa kuelekea kituo cha kimataifa cha anga za juu.
Watafiti wanasema nyaya hizo zinazotumia nguvu za maalum za sumaku ambazo kwa Kiingereza huitwa electro-dynamic, kitazalisha nguzu za kutosha kubadili mwelekeo wa vipande hivyo na kuvielekeza kwenye anga ya dunia ambapo vitateketea.
Kampuni ya wataalamu wa kuunda nyavu za kutumiwa na wavuvi Nitto Seimo Co, ambayo imekuwepo kwa miaka 106, imeshirikiana na shirika la anga za juu la Japan kuunda mtambo huo.
Majaribio ya kutumia mtambo huo ni moja ya juhudi za kuhakikisha anga za juu ni salama kwa wana anga kwa kupunguza taka.
Inatarajiwa kwamba itasaidia kulinga vituo vilivyo anga za juu pamoja na setilaiti za kutabiri hali ya hewa na zile zinazotumiwa kwa mawasiliano, vyote vya thamani ya mabilioni ya dola.
Wataalamu wanasema kuna manufaa mengi yatakayotokana na kuondolewa kwa taka kwa kutumia mradi huo wa Japan, lakini wanasema huenda ukafanikiwa kwa vipande vikubwa pekee vya taka.
0 Maoni:
Post a Comment