Karim Benzema kwa sasa anaumri wa miaka 29 na ni raia wa Ufaransa, nafasi yake uwanjani ni mshambuliaji. Benzema kwa sasa yupo katika klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania, ambayo amedumu nayo kwa jumla ya misimu 8 ya mpira.
katika gazeti la Daily Star Arsenal wamerudisha nguvu kumuwinda Benzema, hii hatua waliifanya mwaka 2013.
Habari zilizopo ni kwamba Benzema huenda akaihama klabu ya Real Madrid katika kipindi cha kiangazi na kujiunga na timu ya Arsenal ya nchini uingereza.
Real Madrid imepanga kumuuza Benzema kwa gharama kubwa. Real pia imeweka macho yake katika kusajili mshambuliaji chipukizi kuchukua nafasi ya Benzema kutoka kwa Pierre Emerick, Aubameyang na Paulo Dybala
PSG na Chelsea nao wanaitaka saini ya Benzema.
0 Maoni:
Post a Comment