Watu wenye ulemavu wa ngozi yaani ALBINO wamepokea vifaa
pamoja na elimu kuhusu matumizi ya vifaa na mafuta ambayo huwakinga na mwanga
mkali unaotokana na miale ya jua kali. Hayo yamefanyika leo hii katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa wakati wakipewa maelekezo na jinsi ya
kutumia mafuta hayo ya ngozi ambayo yanawalinda kutokana na miale ya jua.
Katibu wa watu wenye ulemavu (TAS)
Dr
Pilly Shing’oma akitoa maelekezo
Wanafunzi wakipakana mafuta aina ya Kilimanjaro Suncare
Dr Pilly Shing’oma ni daktari anayehusika na magonjwa ya ngozi
na Albino ikiwa ni mojawapo, amesema watu
wenye ulemavu wa ngozi wapo wengi mkoani hapa na mafuta hayo wanayowapa
yanauzwa kwa gharama kubwa japo wao wanatoa bure katika clinic zao zote
zinazotoa Huduma hizo. Pia Dr. Pilly amewaomba wazazi na walezi pamoja na watu
wengine wenye ulemavu huo wa ngozi kujitokeza kwenda katika vituo hivyo vya
Afya ili kuweza kupatiwa misaada mbalimbali pamoja na matibabu ya ngozi. Lakini
pia Aliongeza kwa kutoa wito kwa wanajamii kuto amini katika imani za
kishirikina kwamba viungo vyao vya mwili kutumika katika kuleta utajiri na kua huo ni
uongo ambao unafanywa na baadhi ya waganga wa jadi.
Katibu wa Chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi (TAS) Mkoa wa
Iringa bwana Leo Sambala amewashukuru shirika la USAID kuwapatia vifaa vinavyowasaidia kuto athirika na mionzi ya
jua wakiwa wanafanya shughuli zao. Aidha katibu huyo amewaomba Walimu
kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi ambao wako mashuleni kutotoa adhabu
kali kwa wanafunzi hao kwa kuwaweka juani na pia kuwapa kipaumbele kwa kuwaweka
darasani viti vya mbele ili waweze kuona maandishi ambayo yameandikwa na kuwapa
notes ambazo zina maandishi ambayo wanaweza kuyasoma kwa urahisi.
Watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa Iringa wapo karibu 350 ambao
wanaishi sehemu mbalimbali za Mkoa huu na baadhi yao wamekua ni vigumu kupatiwa
misaada hiyo kutokana na wengine kukaa shemu za mbali na pia hali ngumu ya
maisha yao inawafanya kukosa nauli za kuweza kusafiri kuja kuchukua huduma
hizo.
Hivi karibuni hakujaripotiwa kuwepo kwa mauaji ya Watu wenye
ulemavu wa ngozi yaani ALBINO kuuawa na hii inamaanisha kua elimu imewezqa
kuwafikia watu wengi zaidi na wameelimika tofauti na ilipokua mwanzo kulipoku
kunaripotiwa mauaji mengi zaidi ya watu
hawa wenye ulemavu wa ngozi.
0 Maoni:
Post a Comment