Moja
ya habari ambazo zimetawala katika mitandao mingi ya kijamii kwa
Alhamisi ya Novemba, 3 ni habari ambayo inamhusisha model aliyetumika
katika nyimbo ya Diamond Platnunz na Rayvanny – Salome kuwa amepoteza
maisha kufuatia kutekwa, kubakwa na kuuliwa kisha mwili wake kutupwa
mtaroni.
Taarifa
iliyokuwa katika mitandao imemtaja model huyo kuwa jina lake Juliana
lakini kipindi cha XXL cha Clouds Fm kimemtafuta model huyo
na amekanusha kuwa sio yeye ambaye amefariki na jina lake sahihi ni
Lillian na ameshtushwa na habari hizo kwani hamfahamu hata mtu
aliyekutwa na mkasa huo.
0 Maoni:
Post a Comment