Na, Dajari Mgidange
Imeelezwa kua kuna baadhi ya wananchi wamekua wakitumia
vibaya namba za dharura kwa kupiga namba hizo bila ya kua na tatizo lolote
ambalo wangetakiwa kusaidiwa na mamlaka husika.
Hayo yamezungumza na Kamanda wa Jeshi la Zima moto Mkoa wa
Iringa Bwana Kennedy Komba alipokua akizungumza na Matukio Daima amesema
wamekua wakipokea simu mbalimbali ambazo sio rasmi kutoka kwa baadhi ya
wananchi huku wakidhani wanapokea matukio ya moto kitu ambacho sio sahihi.
“Tumekua tukipokea simu mbalimbali wakisema vitu ambavyo hata
havihusiani na zima moto simu yetu inaruhusu kupokea simu moja tu sasa wakati
wakipiga simu hiyo kunakua labda na mhanga ambaye kwa wakati huo angehitaji
kusaidiwa hivyo hawezi kusaidiwa kwa wakati”. Alisema Komba.
Aidha Komba amesema kua tayari wameanza kushirikiana na Jeshi
la Polisi ili kuweza kuwabaini watu hao wanao tumia namba vibaya ya zima moto
na punde watakao kamatwa watafunguliwa mashitaka na kupelekwa mahakani.
Komba amewataka wananchi kuweza kutumia namba hiyo ya 114
ambayo inatumika kupokea matukio na majanga ya moto kutoka kwa wananchi ili
kuweza kuripoti matukio hayo muhimu na sio kueleza mambo mengine ambayo
hayahusiani na jeshi hilo la zima moto, Akitolea mfano Komba alisema, “Kuna mtu
alipiga simu akasema hapo ni Zima moto na Akasema kua alikua anajaribu kua kama
hua tunapokea simu”.
0 Maoni:
Post a Comment