Makonda azidi kuwabana wenyeviti wa Mitaa Amburuza mwingine rumande



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana  aliliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Zavala kata ya Buyuni Ilala, Chiku Said baada ya kutuhumiwa kuuza viwanja vya watu pamoja na serikali kinyume na sheria.

Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi kulalamika kwa kumtuhumu mwenyekiti huyo kuuza viwanja vya serikali kinyume na sheria bila kuwahusisha wajumbe wenzake hali ambayo imesababisha mgogoro mkubwa wa ardhi katika eneo hilo

Hatua hiyo ilimfanya mkuu wa mkoa  kumtaka Afisa Ardhi wa Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela kuthibitishwa kuuzwa kwa eneo hilo kinyume na sheria.

“Mkuu wa mkoa, ni kweli tulikuwa na eneo Block J lakini limeuzwa,” alisema afisa huyo “Nataka kuwaambia kitu wenyeviti wa mtaa hawaruhusiwi kuuza eneo katika mtaa. Mimi ningewataka wenyekiti kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa ili kuepuka kutokea kwa hayo mambo,”

Baada ya kauli hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,  Makonda akaliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi
 
 
 
 
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment