Maisha ya nyota wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard katika klabu ya Marekani ya LA Galaxy inayoshirikia ligi ya MLS yamefikia tamati ikiwa ni msimu wake wa pili tangu kujiunga na timu hiyo ambayo alimsajili mwaka jana.
Gerrard ameandika ujumbe wa kuwaanga mashabiki wa LA Glaxy kupitia ukurasa wake wa Instagram, “Sehemu nzuri na yenye mwonekano mzuri, nitawakumbuka LA.”
Kwa kipindi chote ambacho Gerrard ameitumia klabu hiyo, amecheza michezo 34 na kufunga magoli matano
Licha ya maisha yake ya soka katika klabu ya LA Glaxy kumalizika, bado haijafahamika moja kwa moja kuwa Gerrard atajiunga na klabu gani au atakuwa amemaliza maisha ya soka japo kuwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp aliwahi kuzungumza kuhusu Gerrard kama ana nafasi ya kurejea katika klabu hiyo aliyoitumikia kwa miaka mingi.
“Huwezi kufikiria jinsi atakavyo karibishwa. Hakuna tatizo, lakini kila kitu tayari tunacho na tutazungumza nae kuona inakuwaje kuhusu jambo hilo,” alisema Klopp.
Aidha taarifa zisizo rasmi zinasema kuwa klabu ya Newcastle United inataka kumsajili Gerrard na anaweza kujiunga mwezi Januari katika dirisha dogo la usajili.
0 Maoni:
Post a Comment