MWILI WA MUNGAI KUAGWA DAR LEO

MWILI wa aliyewahi kuwa Waziri na Mbunge katika Jimbo la Mufindi Kaskazini, Joseph Mungai (73) utaagwa leo katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam na kisha kusafirishwa kwenda Mafinga mkoani Iringa kwa ajili ya maziko yatakayofanyika Jumamosi.

Mtoto wa tatu wa marehemu, William Mungai alisema hayo jana nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam. William alisema familia imempoteza Mzee Mungai juzi jioni baada ya kuugua kwa muda mfupi saa 10 jioni.

“Kwa sasa utaratibu tuliopanga ni kwamba kwa kuwa mzee alitumia muda mrefu akiwa mbunge kule Mufindi takribani kwa miaka 35, hivyo tutaenda kumpumisha kule maana ndio nyumbani,” alisema William.

Alisema baada ya ratiba ya kuaga, familia itaondoka kwenda Mafinga ambako ndipo watakapompumzisha Jumamosi saa nane mchana. Alisema kwa wakazi wa Mafinga nao watajumuika kutoa heshima zao za mwisho kesho, lakini Jumamosi ndio atazikwa.

William alisema ni ugonjwa wa ghafla, lakini bado wanashauriana na daktari wake, alikuwa akimtibu tumbo maana Mzee Mungai alikuwa akilalamika kuumwa na tumbo.

Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema atamkumbuka Mungai kama mwanasiasa mkongwe aliyekuwa amebaki hata kwa Mkoa wa Iringa. Alisema ni kiongozi ambaye amewahi kuwatumikia Watanzania katika awamu zote na akiongoza wizara mbalimbali.

Mwanasiasa mkongwe, Chrisant Mzindakaya alisema ni masikito makubwa sana kuondokewa na Mungai kwani alifahamiana naye kuanzia miaka ya1970. Alisema Mungai alikuwa waziri kijana kuliko wote nchini wakati wa uhai wake akiwa na umri wa miaka 29 na amekuwa wakishauriana katika mambo mbalimbali ya siasa.

Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment