Mgombea mwenza wa Donald Trump katika uchaguzi mkuu wa Marekani uliomalizika kwa Trump kuibuka na ushindi, Hillary Clinton kutoka chama cha Democratic amezungumza kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa kwa matokeo ya kushindwa kwake katika uchaguzi wa nchi hiyo.
Akizungumza kwa hisia, Clintonamesema amehuzunika kutokana na matokeo ambayo amayepata kwani alijiandaa kwa muda mrefu na matarajio yake ilikuwa na kuibuka na ushindi ili kuwa raia wa 45 wa Marekani na kuwa rais wa kwanza mwanamke kuongoza taifa hilo kubwa duniani.
Clinton amesema haina budi kukubali matokeo na kuwa Donald Trump ndiye rais wao anayefuatia baada ya Barack Obama kumaliza muda wake hivyo ni vyema Wamerekani wakungana kwa pamoja kufanya kazi na Trump kwani kwa sasa kuna mgawanyiko ambao unawagawa wananchi wa nchi hiyo.
“Tunaona kuwa nchi yetu imegawanyika sana kuliko tunavyofikiri lakini bado nina imani na Marekani na nitaendelea kuamini na kama na wewe unaamini basi inabidi tukubali na tuendelee na ujenzi wa taifa, nimempongeza Donald Trump na kupendekeza kufanya kazi pamoja kwa niaba ya taifa letu. Naamini atakuwa rais mwenye mafanikio kwa Wamarekani wote,
Donald Trump anakuwa rais wetu, tunatakiwa tumpe nafasi ya kuongoza, demokrasia yetu katika katiba inasisitiza kupeana madaraka kwa amani, na hatuheshimiani pekee bali tunajivunia hilo na tunahakikisha utawala wa sheria na kanuni. Haya hayakuwa matarajio yetu ambayo tulikuwa tukiyataka na tulifanya sana kazi ili hilo litimie, samahani hatujaweza kushinda uchaguzi,” alisema Clinton.
0 Maoni:
Post a Comment