Kocha mpya wa Yanga George Lwandamina atatambulishwa rasmi kesho (Ijumaa Novemba 25) saa 5:00 asubuhi makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Twiga na Jangwani-Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Yanga pia itamtambulisha Hans van der Pluijm kama Technical Director wa klabu hiyo baada ya ujio wa Lwandamina ambaye amechukua nafasi ya ukocha mkuu kwa mabingwa hao watetezi wa taji la VPL.
Inaelezwa wawili hao watatambulishwa na Clement Sanga Makamu Mwenyekiti wa Yanga.
0 Maoni:
Post a Comment