Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu, IS, jumamosi iliyopita wamewauwa askari wa zamani wa vikosi vya usalama vya Iraqi wapatao 40, katika eneo karibu na mji wa Mosul na kutupa miili yaao katika mto Tigris.
Msemaji wa masuala ya haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Ravina Shamdasani, Jumanne hii (01.11.2016) ametoa taarifa hiyo, akiangazia ripoti kutoka eneo lilipotokea tukio hilo.
Taarifa kutoka Umoja wa Mataifa, Geneva zinaeleza kwamba kundi hilo la Dola la Kiislamu pia lilijaribu kuwasafirisha raia 25,000 kutoka Hammam al-Alil, mji ulioko Kusini mwa Mosul, wakiwa kwenye malori na mabasi madogo wakati kulipoanza kuingia giza, mnamo siku ya jumatatu, na lengo lao likidhaniwa kuwa ni kuendelea kuwatumia raia hao kama ngao ya vita kwenye maeneo yao yanayolengwa na majeshi, Shamdasani amesema.
Amesema, hatua hiyo moja kwa moja inadhihirisha kwamba wanataka kuwatumia raia hao kama ngao ya vita, pamoja na kujihakikishia kwamba eneo lao linakuwa na raia wengi ili kuyafanyia ugumu majeshi ya usalama katika operesheni yake ya kuwafurusha na kuukomboa mji wa Mosul. Wamekuwa pia wakiwauwa baadhi ya watu waliowateka, hususan wale waliowahi kuwa askari wa jeshi la Iraqi.
Askari hao 40 wa zamani waliouwawa Jumamosi iliyopita walikuwa ni kati ya raia waliowateka mapema katika wilaya ndogo ya Mosul, al-Shura, pamoja na vijiji vingine vinavyozunguka Hamman´m al-Alil.
Kwingineko huko Iraqi, inaarifiwa kuwa vikosi vya usalama va Iraqi vimeingia kwenye viunga vya Mosul, na kulikamata jengo lenye kituo cha televisheni cha Mosul, kama sehemu ya mashambulizi hayo ya kuwaondoa wapiganaji wa Dola la Kiislamu kutoka kwenye mji huo, chanzo cha habari cha jeshi kimesema.
0 Maoni:
Post a Comment