Godbless Lema Afikishwa Mahakamani Arudishwa Rumande Baada ya Kunyimwa Dhamana


Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema jana amefikishwa mahakamani mkoani Arusha na kusomewa shtaka la uchochezi kwa viongozi wa serikali.

Lema amefikishwa mahakamani akiwa tayari amekaa rumande takribani siku 7 tangu alipokamatwa.

Lema anakabiliwa na shtaka la uchochezi ambapo ni pamoja na kumtishia Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kauli yake aliyoitoa dhidi ya Rais Dkt Magufuli kuwa Mungu amemuonyesha asipojirekebisha atafariki.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, Lema amerejeshwa rumande baada ya kukosa dhamana kufuatia pingamizi lililowekwa na upande wa Jamhuri.

Mahakama imeeleza kuwa itatoa uamuzi kuhusu dhamana ya Lema Novemba 11 mwaka huu.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment