JPM ATOA MAAGIZO MANNE BANDARINI

Rais
Magufuli ameagiza mkataba wa kampuni ya Ticts inayopakia na kuondosha
mizigo bandarini ufanyiwe marekebisho ili kulinufaisha Taifa kutokana na
oparesheni zake bandarini.
Vilevile ameiagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) inunue mashine nne za kukagulia mizigo inayoingia bandarini hapo.
Ameitaka TPA na waziri husika kufunga floor meters ndani ya miezi minne.
Pia TPA ijenge bandari kavu Mlandizi na kutozitumia binafsi zilizopo kwakuwa zinatumika kukwepa kodi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa
vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson
Msigwa imeeleza hayo alipokutana na wafanyakazi wa bandari.
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
0 Maoni:
Post a Comment