BURUNDI WATOA MSAADA WA CHAKULA KAGERA
Serikali
ya Burundi imetoa msaada wa vyakula kwa waathirika wa tetemeko la ardhi
mkoani Kagera na kuvikabidhi kwa viongozi wa mkoa huo wakiongozwa na
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Dk Suzan Kolimba aliyeiwakilisha Tanzania
Waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi,
Leontine Nzeyimana akikabidhi msaada huo leo wilayani Ngara amesema
msaada ulitolewa na nchi hiyo ni mchele tani 100, mahindi tani 50,
sukari tani 30 na majani ya chai tani tatu.
Nzeyimana amesema wakazi wa Kagera
waliokumbwa na tetemeko hilo ni ndugu wa wananchi waliko nchini Burundi
hivyo nchi imeguswa na na athari hiyo na kwamba msaada huo ni kidogo
lakini upokelewe kwa lengo la kukuza mahusiano na ujirani mwema.
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
0 Maoni:
Post a Comment