Wanairinga wampongeza
Askofu kutimiza miaka 25 ya Uaskofu
Na, Dajari Mgidange
Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni pamoja na mch. Msigwa
Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa
Rais mstaafu Benjamini Mkapa
Sherehe
ambazo zilifanyika katika viwanja vya kanisa la Roman Catholic Kihesa tar 1
Julai 2014 kumuaga Askofu Tarcisius J.M Ngalalekumtwa zikiwa zimeambatana na
baadhi ya viongozi wakubwa wa Serikali. Baadhi ya viongozi hao ambaye mgeni rasmi alikua ni Mh. Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter
Pinda na wengine ni Mh. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna
Makinda, Rais Mstaafu Mh. Benjamini William Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Ngoyai Lowasa, Mkuu wa Mkoa wa
Iringa Dr. Christine Ishengoma, Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mch. Peter
Msigwa pamoja na Mbunge wa viti maalum Iringa Ritha Kabati na viongozi wengine
wa Kisiasa.
Makamu Raisi
Baraza la Maaskofu Tanzania Bw.Severine Rweguzi alisema kutimiza Miaka 25 ya
Uaskofu ni furaha kwetu sote tangu Januari mwaka 1989 mpaka sasa 2014.
“Mchungaji mwema hujitoa uhai kwaajili ya kondoo wake na wewe ni Mchungaji
mwema umehudumu nafasi mbalimbali tangu uongozi wa Msekwa”, Alisema Askofu. Pia
aliongeza kwa kusema tangu aliposhika nafasi ya Uaskofu amekua mwema, mkarimu
na mwenye misimamo imara na kwahilo wamemshukuru pamoja na kuwepo na baadhi ya
changamoto mbalimbali na mengi ameyashuhudia Mema , Mabaya na kukatishwa tama
lakini alisimama imara pamoja na mabati meupe aliyokua nayo kichwani hakika
yeye ni Jembe Jembe la Kanisa, Mungu
azidi kukubaliki ili uzidi kutenda vyema.
Pia
aliongeza kwa kugusia Serikali na kusema kua, “Tumeshuhudia mambo mengi ya aibu
ambayo yanaendelea ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo
baadhi ya Wabunge hawajiheshimu na sasa sisi Wananchi tuko njia panda kama
Katiba itapatikana au haitapatikana na ninawaomba Wabunge wa Upinzani waweze
kurejea bungeni na kukuamilisha Katiba”.
Mgeni rasmi
ambaye ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda ambaye alikaribishwa na
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma alisema, “Mwaka 1988
alipoteuliwa katika ngazi hii ya Uaskofu alikwenda Ruvuma na tulishukuru sana
kwa ujio wake lakini muda mfupi tukasikia amehamishiwa Iringa. Nimesikia kua
kichwani una mvi lakini mimi naona badotunakuhitaji kutokana na mazuri mengi
uliyofanya kwa kua na Mashehe Masi 6 wanaotarajiwa kua Maaskofu pia Maseminari
200, shule za msingi, Shule za sekondari 6, Chuo cha ufundi na kuhakikisha kua
na chuo kikuu kishiriki RUCO pamoja na vituo vya afya 6”.
Pia
mheshimiwa Waziri Mkuu alimsifu kwa kua na mvuto katika watu na akamtaka Askofu
kuwaombea kutokana na mambo yaliyo ndani ya siasa yao. Kuhusu Katiba Mheshimiwa
Mizengo alisema bado tunahitaji Katiba itakayotuongoza kwa miaka mingi zaidi
ijayo na kwa kuwa mwamuzi wa mwisho ni Mwananchi, ambaye ataamua kwa kupiga
kura ya maoni.
Sherehe hizo
ziliambatana na zawadi mbalimbali pamoja na kuhudhuliwa na baadhi ya maaskofu
wengi kutoka kila pembe ya nchi na wananchi wengi kufurika eneo hilo huku
kukiambatana na ulinzi mkali kwa kukaguliwa kwa kila mwananchi aliyekua
akiingia viwanjani hapo.
0 Maoni:
Post a Comment