Mfumo mpya wa Biometric
Voter Registration(BVR) kutumika kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura kwa
awamu ya Kwanza
Na, Dajari Mgidange
Jaji mstaafu kulia John Mkwawa
Denis Mlowe akiuliza swali kwa Tume
Akizungumza na waandishi wa habari kamishna wa Tume yaTaifa
Uchaguzi Mheshimiwa Jaji John J. Mkwawa katika ukumbi wa mkutano wa Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Iringa jana tarehe 02
Julai 2014, alisema kuwa Tume inatarajia kufanya uboreshaji wa Daftari la
kudumu la Wapiga kura kwa awamu ya kwanza hivi karibuni kwa kutumia Teknolojia
mpya ya Biometric Voter Registration (BVR).
Jaji aliongeza kwa kusema kwamba, “Mfumo wa Biometric Voter
Registration (BVR) ni mfumo wa kuchukua au kupima taarifa za mtu za Kibaolojia
au tabia ya mwanadamu na kuzihifadhi katika kanzi Data (Database) kwaajili ya
utambuzi. Mfumo huu hutumika katika kumtambua binadamu na kumtofautisha na
mwingine. Taarifa za mtu za kibaolojia au tabia za mwanadamu ziko nyingi hata
hivyo kwaajili ya kuandikisha wapiga kura alama za vidole kumi(10) vya mikono,
picha na saini ndizo zitakozochukuliwa na kuhifadhiwa kwenye kanzi Data
(Database) ya wapiga kura. Kwa kutumia mfumo huu mpya wa BVR, Wananchi wote
wenye sifa za kuwa wapiga kura na wale walio na kadi za mpiga kura watatakiwa
kuandikishwa upya”.
Pia Jaji alisema kua mfumo huu utasaidia kuwa na Daftari
sahihi na linaloaminika zaidi kwaajili ya upigaji wa Kura ya maoni na uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2015 na Tume inapenda ieleweke kwamba Biometric Voter
Registration Kit (BVR-Kit) itatumika tu kwaajili ya kuandikisha wapiga kura na
sio vinginevyo. Uamuzi wa matumizi ya BVR umefikiwa kutokana na changamoto
zilizojitokeza katika matumizi ya Teknolojia ya Optical Mark Recognition (OMR).
Matumizi ya OMR yalisababisha kwa kiasi kikubwa Daftari la kudumu la wapiga
kura kua na Kasoro.
Na Mkurugenzi Idara
ya Habari NEC Bi Ruth Masham aliongeza
kwa kusema Biometric Voter Registration (BVR) ni mfumo wa kuchukua au kupima
taarifa za mtu za kibaolojia au tabia ya mwanadamu na kuzihifadhi katika Kanzi
Data (Database) kwaajili ya utambuzi. Matumizi makubwa ya Teknolojia hii ni
kujaribu kujibu maswali makubwa mawili, huyu ni nani na je ni kweli huyu ndiye
yeye. “Kuna aina mbalimbali za biometric features ambazo zinaweza kutumika
katika kumtambua mtu na kumtofautisha na mwingine kama vile, alama za vidole,
sura, mpangilio wa mikono, mboni ya jicho, sauti, saini ya mtu, mwendo na
harufu, lakini kwaajili ya kuandikisha wapiga kura alama za vidole vyote
kumi(10), picha na saini ndizo zitakazochukuliwa na kuhifadhiwa kwenye Kanzi
Data ya Wapiga Kura”.
Moja ya maswali yaliyoulizwa na baadhi ya waandishi wa habari
waliokusanyika katika kikao hicho ni pamoja na mwandishi Frank Leonard ambaye
aliuliza ni kiasi gani cha watu wanatarajiwa kuwaandikishwa na kujibiwa na Jaji
John Mkwawa kuwa wanaotarajiwa kuandikishwa ni milioni 20 na walioongezeka ni milioni
6 kwahiyo jumla yao ni Watanzania milioni ishirini na sita (26)
Wananchi wametakiwa kwenda kwenye vituo vya kujiandikisha
pindi muda utakapowadia na kujiandikisha kwani ni muhimu sana na vitambulisho
vya kupigia Kura vitatolewa vipya na zoezi zima la kujiandikisha litadumu kwa
muda wa siku kumi na nne(14) au wiki mbili Kwenye vituo vyao vya kupiga Kura.
0 Maoni:
Post a Comment