Wananchi watakiwa kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru
Na, Dajari Mgidange
MKUU WA MKOA DR.CHRISTINE ISHENGOMA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI

BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WALIOHUDHURIA

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo tar 23/06/2014 saa tano asubuhi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh.Dr.Christine Ishengoma, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuulaki mbio za Mwenge utakaoanza tar 24/06/2014 ukitokea mkoani Morogoro ambao utapokelewa mpakani mwa Iringa na Morogoro  Ruaha Mbuyuni na Mkuu wa Mkoa kuanzia saa 2.00 hadi saa 3.00 asubuhi.
Baada ya kupokelewa Mwenge wa Uhuru kutoka mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Mkoa wa Iringa atamkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kilolo ili aweze kuukimbiza katika Wilaya yake na baada ya Kilolo Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa tar 25 juni, 2014 Manispaa ya Iringa utakimbizwa tar 26 juni, 2014 na Halmashauri ya wilaya ya Mufindi utakimbizwa tarehe 27 juni, 2014 kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 3.00 asubuhi. Baada ya Mwenge wa Uhuru kukimbizwa katika mkoa wa Iringa utakabidhiwa kwa Mkoa wa Njombe tarehe 28 juni, 2014
Shughuli ambazo zitafanywa na Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Iringa ni kukagua Miradi ya Maendeleo, kuweka mawe ya msingi na kufungua pamoja na kuzindua miradi ya maendeleo 42 yenye thamani Tsh. 3,109,958,020/=. Lakini pia Mwenge wa Uhuru utatoa ujumbe katika maeneo yote ambako utakimbizwa. Miradi ambayo itatembelewa na Mwenge wa Uhuru  ni miradi ya Barabara, Miradi ya Maji, Miradi ya Afya, Miradi ya Kilimo na Ufugaji, Miradi ya Vijana na Wanawake na Miradi ya hifadhi ya Mazingira.
Mwenge wa Uhuru utabeba ujumbe maalumu ambao hukusudiwa kuwasilishwa kwa wananchi kuhusu jambo muhimu linalohusu Taifa katika wakati uliopo. Ujumbe maalum wa mwenge wa uhuru kwa mwaka 2014 unasema, “Katiba ni Sheria kuu ya Nchi” wenye kauli mbiu jitokeze kupiga kura ya maonitupate katiba mpya sambamba na ujumbe maalum. Mwenge wa uhuru hua kila mwaka unatoa Elimu na kuhamasisha wananchi kupambana na maadui watatu wa maendeleo ambao ni Rushwa, Matumizi ya Dawa za kulevya na Ugonjwa wa UKIMWI.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa amewasihi wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu wakati  wote ambapo Mwenge wa Uhuru utakua ukikimbizwa katika Mkoa wetu na hata baada ya kuhitmisha Mbio za Mwenge katka Mkoa wetu. 
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment