Wananchi waaswa kutowanyanyasa Watoto
Iringa
Picha na Dajari Mgidange
Akizungumza na Wananchi pamoja na watoto waliohudhuria katika
sikukuu ya mototo wa Afrika katika viwanja vya Mwembetogwa vilivyopo kata ya
Makorongoni mjini Iringa, Mh. Meya Amani Mwamwindi amewataka Wananchi siku ya mototo
wa Afrika kupinga utumikishwaji wa watoto katika ajira mbaya, mauaji ya Albino,
Ubakaji, Ulawiti, Vipigo na kutelekezwa watoto na wazazi.
“Maadhimisho haya hufanyika kila mwaka kwa lengo la
kuikumbusha jamii haki za watoto. Tukio hili ni kubwa lina umuhimu wake katika
manispaa yetu, Taifa na Kimataifa tukio hili ni kumbukumbu ya watoto wapatao
15,000 waliouwawa na makaburu huko Soweto Afrika Kusini tarehe 16/06/1976
wakipinga maamuzi ya serikali hiyo kuwafundisha watoto lugha ya Kikaburu”. Alisema
Mh. Meya.
Pia alioongeza kwa kusema, ”Kila mwaka katika maadhimisho
haya huambatana na kauli mbiu, kauli mbiu ya mwaka huu inasema KUPATA ELIMU
BORA ISIYO NA VIKWAZO NI HAKI YA KILA MTOTO, Kauli mbiu hii imetilia mkazo kwa
wazazi, walezi, familia, serikali na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na
shughuli za maendeleo ya watoto kwa kuliangalia kundi hili, kuhakikisha
wanapata haki zao za msingi za kupata elimu bila vikwazo kwa msingi kwamba
mtoto awapo shuleni hatakiwi kunyanyaswa kwani haki yake yeye ni kusoma na
kupata Elimu, masuala ya ada, michango mbalimbali nijukumu la mzazi au mlezi,
kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watoto kurudishwa majumbani pale mtoto
anapokua hajakamilisha baadhi ya michango au ada ,hilo ni jukumu la wazazi”.
Regina Mushi ambaye ni mzazi alisema siku ya mtoto wa Afrika ni siku nzuri kwa watoto kwani
imeweza kuwakutanisha pamoja na kujadili changamoto zao pamoja. Pia kumekuepo
na changamoto ya baadhi ya wazazi/ walezi kuwafungia watoto ndani na mwingine
aliweza kumfungia mtoto kwenye boksi na hatimae baadae kufariki, Bi Regina
alisema, “tukio hilo ni baya na pia ni kama changamoto kwa wazazi kwani watu
wote waliweza kuliona tukio lile kwahiyo wanapokutana na matukio kama hayo au
wanapoona waweze kuripoti katika vituo vya polisi”.
Pia mtoto Henry Mwalongo alisema,”siku ya motto wa Afrika
inawahimiza wazazi kutowanyanyasa watoto hasa katika swala la elimu kutupatia
elimu isiyo na vikwazo vya aina yoyote ile”. Pia Bw. Tonny Adamms kutoka
kiwanda cha ASAS Dairies alisema kua wao wakua wakishiriki katika matamasha
mbalimbali likiwemo hili la watoto na hata yanayo wahusu vijana napia wameweza kutoa maziwa paketi mia
tano(500) kwa watoto walioshiriki siku hiyo na pia kiwanda cha pipi cha Ivory waliweza
kutoa pipi 600. Na kuweza kuwapatia watoto wote walioweza kushiriki katika siku
hiyo.
Sikukuu hii huweza kuadhimishwa kila mwaka ya tarehe 16 mwezi
wa 06 ya kila mwaka barani Afrika ambayo kihistoria iliwekwa kutokana na watoto
walioweza kupoteza maisha yao nchini Afrika ya kusini ambao walikua
wakiandamana kupinga lugha wanayofundishiwa huko mashuleni ya Kikaburu na
huweza kuadhimishwa kupinga ukatili na unyanyasaji wa watoto barani Afrika.
0 Maoni:
Post a Comment