MTOTO ALIYEDAI WA LOWASSA AKAMATWA NA POLISI


Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema wanamshikilia Fatuma Chikawe kwa tuhuma za kudanganya kuwa ni mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.

Hii ni wiki moja baada ya Fatuma kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kudai ametelekezwa na Lowassa kwenye zoezi la kusikiliza malalamiko ya wanawake waliotelekezewa watoto linaloendeshwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ambaye alisisitiza wahusika watoe taarifa za ukweli.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment